VIDEO>Simba, bado alama mbili kutwaa ubingwa wa Tanzania
Mshambuliaji kutoka Uganda, Emmanuel Okwi amefunga bao muhimu na kuipa Simba alama tatu muhimu kuelekea kampeni ya kutwaa taji la Ligi Kuu Tanzania Bara
Simba imeishinda Ndanda bao 1-0 ambalo lilifungwa na Okwi dakika ya 40 ya mchezo baada ya kuwatoka mabeki wa Ndanda na kuachia shuti kali lililomshinda kipa wa Ndanda.
Bao la Okwi limemuwezesha kufikisha idadi ya mabao 20 aliyofunga msimu huu na kuwa kinara wa ufungaji mabao.
Simba imefikisha alama 65 na inahitaji alama mbili tu ili itangazwe bingwa wa ligi kuu tanzania Bara msimu wa 2017/18.
No comments